Uswahili

Deno Sparta

Member
KCr.
0.00
KAZI ZA TEZI DUME NAUMUHIMU WAKE KWA MWANAUME

TEZI DUME (Prostate gland)

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

KAZI ZA TEZI DUME AMBAZO ULIKUWA HUZIJUI;

1. Tezi dume hutoa majimaji ambayo huchanganyika na mbegu za kiume na kutengeneza shahawa. Asilimia 60 ya shahawa huwa ndio hayo majimaji yaliyotengenezwa na tezi dume na asilimia 40 ndio mbegu za kiume zilizotengenezwa kwenye kiwanda cha mbegu(korodani).

2.Majimaji yanayotoka kwenye tezi dume huanza kutangulia mbele kusafisha njia ya mkojo ili kuondoa asidi kwenye njia hiyo na kubakia hali ya alkaline ili mbegu za kiume zisife.hivyo inaondoa asidi na pia inazilinda zisife kuanzia kwenye njia ya mkojo ya mwanaume mpaka ukeni kwa mwanamke maana napo kuna asidi sana.

3.kazi nyingine ya tezi dume ni kuchuja sumu ili zisichanganyike na mbegu za kiume hivyo hata mbegu inakuwa haina ugonjwa na salama

4.Tezi dume ndio yenye kufunga njia ya mkojo na kuruhusu mbegu za kiume zitoke wakati umefika kileleni na kuziba njia ya mbegu za kiume na kufungua njia ya mkojo unapokuwa umemaliza tendo

5.Wanaume tukimaliza tendo huwa shahawa zinaruka sana hiyo ni kazi ya tezi dume. Kama shahawa zako zinamwagika tu lakini haziruki zenyewe kama mkojo nikiwa na maana kwa speed ujue tezi dume lako haliko sawa.pia ngumu mbegu zako kufikia yai la mwanamke na kumpa ujauzito.

6.Tezi dume inailinda njia ya mkojo isishambuliwe na vijidudu vya U.T.I

7. Tezi dume ni sehemu ya kilele cha raha kwenye tendo la ndoa kwa mwanaume.

8.Tezi dume kupitia majimaji yake ndio inayosafirisha mbegu za kiume kutoka kwa mwanaume mpaka kwa mwanamke na kukutana na yai la mwanamke.

9.Majimaji yanayotoka kwenye tezi dume dio chakula cha mbegu za kiume. Kwahiyo mbegu za kiume zinapata chakula kutoka kwenye tezi dume.

Kuvimba Tezi Dume (BPH)
Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba.

Kuvimba kwa tezi dume husababishwa na nini?
Chanzo halisi cha kuvimba kwa tezi au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa ugonjwa huu hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu lakini siku hizi hata vijana.

BAADHI ZA TAFITI ZINAONYESHA KUWA HORMONES,UMRI MKUBWA NA MAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO NI VYANZO VYA KUVIMBA KWA TEZI

DALILI ZA KUVIMBA KWA TEZI DUME:

-Hukojoa mkojo unaokatika katika
-Hukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
-kuchukua muda kabla ya mkojo kuanza kutoka
-Hali ya kujihisi kubanwa na mkojo kila mara
-Kushindwa kuthibiti mkojo kiasi cha mkojo kutirika wenyewe
-Hali ya kuhisi mkojo haujaisha kwenye kibofu
-Hukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
-Kushindwa kukojoa kabisa (urine retention)

BAADHI YA MADHARA YA KUVIMBA KWA TEZI:

-Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo (kidney stones)
-Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
-Madhara katika figo au kibofu
-Shinikizo la damu
-Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
-kupungua kwa nguvu za kiume na kushindwa tendo la ndoa
-Uhanithi
-vifo
- kufeli kwa Figo katika ufanyaji KAZI wake (kidney failure) 0629586901
 
Top