Binti alikuwa mfanya kazi wa kazi za ndani siku moja asubuhi alipokea simu kutoka kwa mwajiri wake.
Boss alisema: "Naomba leo usije kazini nimeshaweka mtu mwingine kwenye nafasi yako.!"
Binti alilia sana maana familia yake ilikuwa inamtegemea na huo mshahara ndo ulikuwa chanzo pekee cha kujipatia riziki.
Wakati analia alisikia sauti za watu waliokuwa wakipita njia huku wakitiana moyo, mtu mmoja alisikika akisema:-
Mshukuru MUNGU kwa kila jambo, MUNGU hawezi akakuacha hivi hivi, shida, taabu na matatizo ni mitihani ya muda tu hivyo kadili unavyoipita ndiyo unasogea kwenye baraka zake, leo umekosa huenda kesho ndo zamu yako usikate tamaa.
Mwingine akasema AMENI ndugu yangu.
Kisha wakapita zao.
Binti aliposikia vile akajipa matumaini, basi alichukua bibilia akapiga magoti akaanza kusali. Alifanya maombi asubuni na jioni, aliomba kila akitaka kulala na kila akiamka, huku akiendelea kutafuta kazi. Kila mtaa, kila nyumba, kila ofisi na kwa kila mtu.
Siku moja wakati yupo mtaani akizurula kutafuta kazi huku akiwa kachoka na nywere pamoja na miguu yake vimechafuka kwa vumbi, mala alikutana na kijana. Binti uyo bila kusita akamuomba kazi uyo Kijana.
Kijana akamwambia:- "Samahani, unaweza kuja ukanisaidia kufanya kazi ofisini kwangu?
mfanyakazi wangu hajaja nasikia amehama na hajanipa taarifa yoyote.!"
Binti akasema: "Sawa, lakini mimi nilikuwa nafanya kazi za ndani na sijui chochote mambo ya ofisi staff.!"
Kijana akamwabia: "Usiwe na hofu nitakufundisha kila kitu."
Binti alienda kumsaidia huyo kijana na kijana alifurahishwa na utendaji wa kazi wa huyo binti akamwajiri na kuwa anamlipa mshahara mkubwa mara 10 zaidi ya ule aliokuwa akilipwa huko alikotoka, na mwisho akamtafutia nafasi shuleni akaanza kumsomesha. Baadaye akapanda cheo nakuwa mkurugenzi wa iyo kampuni, siku moja wakiwa katika kikao kikuu cha kampuni yao alishangaa kumuona yule mwajili wake aliye mfukuza bila sababu akiwa ni mmoja wa wafanyakazi wa chini kabisa katika kampuni yako ambayo yeye ni mkurugenzi mkuu.
Pale pale kwenye kikao, Binti alipiga magoti na kusema:- "Hakika wewe MUNGU ni mwema umejibu maombi yangu, asante MUNGU."
UJUMBE:
Riziki ya mwanadamu ipo kwa mwenyezi MUNGU, wala usiangaike na wanao kucheka nakukudharau. Achana nao maana hawaijui kesho yako itakuwa vipi.
MUNGU wabariki wote watakao sema "AMENI" au kushiriki kuisambaza post hii "amen"